IJUE SERA YA TAIFA YA UWEKEZAJI WA MWANANCHI KIUCHUMI.
TAFSIRI YA WANANCHI
Walengwa wa Sera ya Uwezeshaji ni wananchi. Makampuni ya wananchi ni yale ambayo yamesajiliwa Tanzania ambayo walengwa wanamiliki asilimia isiyopungua hamsini ya hisa zote za makampuni hayo. Sera ya Uwezeshaji itajumuisha wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyakazi na wafanya biashara katika sekta mbalimbali na makundi mengine. Sera ya Taifa ya Uwezeshaji inatoa mwongozo utakaotumika kutafsiri uwezeshaji utakavyokuwa katika sehemu mbalimbali kulingana na mazingira ya sekta husika. Mikakati itakayobuniwa na sekta mbalimbali, itafafanua uwezeshaji utakuwaje katika shughuli moja moja. Kwa mantiki hiyo, ni wajibu wa kila sekta kufafanua na kuchanganua jinsi ya kutekeleza Sera hii kulingana na majukumu yake.
HALI HALISI NA CHANGAMOTO
Ushiriki wa wananchi wengi katika shughuli za uchumi wa kisasa ni duni. Sehemu kubwa ya uchumi huo imeshikwa na wageni au Watanzania wachache kwa maana ya Sera hii. Hali hiyo inapingana na dhana ya kuleta maendeleo yanayonufaisha na kutoa nafasi ya maendeleo kwa wananchi wengi.
Kisiasa hali ya kutokuwa na fursa ya kushiriki kikamilifu
katika uchumi imesababisha malalamiko miongoni mwa wananchi. Wengi wao
wameshindwa kushiriki kwa sababu ya uwezo mdogo kimtaji, ukosefu wa
ujuzi na uzoefu wa biashara pamoja na matatizo yanayohusiana na
kutokukopesheka. Aidha, hali hiyo imechangiwa na kutokuwa na Sera
madhubuti ya kukabili tatizo la uwezeshaji
Home
»
UWEZESHAJI
»
VIJANA NA MIRADI
»
WASITAAFU WETU
» IJUE SERA YA TAIFA YA UWEKEZAJI WA MWANANCHI KIUCHUMI.